Thursday, September 17, 2015

Upendo Nkone Kufanya Kweli 27th September, 2015

‪Mwanamuziki Upendo_Nkone‬, ni mmoja ya wanawake vinara wa muziki wa injili tanzania. Ni mwimbaji aliyedumu saana katika huduma, na sio tu kudumu lakini pia kuendelea kufanya vizuri kila wakati.Kila Album anayoiingiza sokoni huwa ni bora kuliko jana.
Safari hii akiwa anasherekea na kumuadhimisha Mungu kwa Miaka kumi aliyomuwezesha kufanya huduma anakulete Album mpya kabisaa ya‪#‎OMBA_YESU_ANASIKIA‬...
TAMASHA litafanyika CCC upanga siku ya tarehe ‪#‎27_sepember_2015‬.
Katika tamasha hili utapata nafasi ya kushuhudia UPENDO akiimba live kabisaa na kundi mashuhuri la kusifu na kuabudu toka VCCT Mbezi beach lijulikanalo kama RIVERS OF JOY INTERNATIONAL likisimamiwa ipasavyo na Music Director ‪#‎Samuel_Yonah‬. Wasiojua ukali wa Upendo kwenye live music wajiandae kushangazwa
Wengine watakao sindikiza tamasha hili ni pamoja na Boni Mwaitege, Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji, Martha Baraka na wengine wengi..
Usikubali kwa namna yeyote Kukosa.
‪#‎Kiango‬ itaendelea kukupa habari hatua kwa hatua. Stay tuned.

Tuesday, May 19, 2015

Prophetic Conference from 27th to 31st May 2015 at CCC Upanga. Don’t plan to miss this Special Event

Dr. Bernard Nwaka is the presiding bishop of Living Waters Global Churches located in Zambia, Tanzania, Cameroon, Nambia, United Kingdom and Washington DC. A prophet by calling, he runs apostolic and prophetic schools and is the president of Living Waters Bible College. An international conference speaker, Dr. Nwaka has been in ministry for 23 years and is the author of the book “Invading the Babylonian System and many others. Bishop Nwaka together with Bishop Emmah Isong from Nigeria, will be Speaking in Dar es Salaam during the Prophetic Conference from 27th to 31st May 2015 at CCC Upanga. Don’t plan to miss this Special Event

Monday, May 18, 2015

UZINDUZI WA DVD WA KWAYA YA SOLOMONI TEMPLE ULIKUWA HIVI

Jumapili ya jana ulifanyika uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Solomoni temple huko G/mboto. Kama kawaida Kiango Media katika ubora wake ilikuwepo kuendesha Tamasha hilo. Kiango kabla ya Tamasha iliongea na Mwenyikiti, ambaye alisema kuwa utengenezaji wa DVD waliyoizindua umewaghalimu kiasi cha 9m. pamoja na uzinduzi uliofanyika pia kulikuwa na uchangishaji wa fedha kwaajili ya kununulia vyombo vya Mziki pamoja na mini Bus kwaajili ya kuhubilia injili. alisema kuwa wanatamani kuubiri injili ndani na nje ya jiji la Dar hivyo usafiri utawasaidia kwenda huku na huko.

Katika uzinduzi huo ulisindikizwa na kwaya nyingine ambazo zote zilionyesha ubora wa hali ya juu katika kumwimbia Mungu. ilikuwepo kwaya ya wana wa Assaph kutoka Ukonga, The Living fountain kutoka Tabata kwaya ya the Reapers kutoka KLPT kimara na wenyeji waliokuwa wakizindua The solomoni Temple Gongo la mboto. chini ni picha mbalimbali za tukio zima.


Kwaya yaThe living  Fountain kutoka Tabata












                                                                    Wachungaji
                            Kiongozi wa kwaya ya wana wa Assaph kutoka Ukonga
                                           Kiongozi wa kwaya ya The living  Fountain
                                   MC wa tamasha Moses the Director kutoka Kiango Media


                                                        Wana wa Assaph kutoka Ukonga wakiimba


                              Mc na mwimbaji wa kwaya ya the Reapers KLPT Kimara

                                             wanaume  wanaingia kwa mbwembwe

















                 Mchungaji Kiongozi wa TAG Gongo la mboto na mama Mch pamoja na wajukuu
                                               Mgeni mualikwa akifungua DVD
                                         DVD ikiwekwa wakfu na watumishi wa Mungu

                                                                  Mchungaji Kiongozi
Unaweza kuwasiliana nasi Kiango media kwa ajili ya kukushauri au kuanda tukio lako lolote wasiliana nasi kwa 0713494110